Waasi wa Yemen washambulia meli ya mizigo

Shambulizi la kombora lililofanywa na waasi wa Houthi wa Yemen, lililenga meli ya mizigo yenye bendera ya Antigua na Barbuda katika Ghuba ya Aden, ikiwa ni shambulizi la karibuni zaidi kwenye kwa meli katika eneo hilo.

Kombora hilo lilipiga eneo la mbele cha meli hiyo Jumamosi jioni, na kuwasha moto ambao waliokuwemo waliuzima kwa mujibu wa kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Ambrey.

Kombora la pili lililorushwa kwenye meli hiyo liliwakosa watu waliokuwemo kwenye boti ndogo karibu na eneo hilo ambao walifyatua risasi kwenye meli wakati wa tukio,” Ambrey aliongeza kueleza, ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa ndani ya meli hiyo.

Kituo cha operesheni za biashara za baharini cha jeshi la Uingereza, vile vile kimeripoti shambulizi hilo na moto katika eneo moja karibu na Aden, na kusema kinaendelea kushughulikia uharibifu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii