Askari aua mke na ndugu zake kisa aridhi mali

Rosemary Ndlovu, aliyekuwa askari polisi huko Afrika Kusini, alipatikana na hatia ya kuua mpenzi wake pamoja na ndugu zake watano (5) kisha akachukua fedha za bima zao za maisha jumla ya dola za kimarekani 93,000 kati ya mwaka 2012-2018.

Kabla ya kutekeleza mauaji hayo, Rose alikuwa anatengeneza ukaribu na ndugu husika kiasi cha kujiandikisha kuwa mnufaika wa pesa za bima ya maisha endapo ndugu huyo atafariki. Ndugu walimuamini kwasababu alionekana kuwa ni polisi mwema.

Rose alinaswa baada ya kujaribu kumwajiri muuaji wa kulipwa “hitman” ili awaue dada yake na watoto 5 wa dada yake kwa kuwachoma moto.

Jamaa aliyepewa hiyo kazi akawaonea huruma hao watoto. Aliona ingawa yeye ana roho mbaya kutokana na kazi zake za kukodiwa…ila akagundua Rose ana roho nyeusi…giza kabisa. Jamaa akaamua kumzunguka Rose na akaenda kuwataarifu polisi kuwa polisi mwenzao anaua ndugu zake.

Mwaka 2021 Rosemary akahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii