wachimba migodi 30 wakwama chini ya ardhi kwa siku nne

Makumi ya watu walioajiriwa na kampuni ya uchimbaji madini walikuwa wakifanya kazi katika mgodi mkubwa katika kijiji cha Galkogo, wilayani Shiroro, Jumapili jioni wakati ajali hiyo ilipotokea, amesema Abdullahi Baba Ara, mkuu washirika la uchimbaji madini la Nigeria (SEMA) katika Jimbo la Niger.


"Kulingana na taarifa tulizonazo, zaidi ya wachimba migodi 30 wamenasa kwenye mgodi ambao uliwaangukia walipokuwa wakifanya kazi ndani yake," Bw Ara amesema. "Watu saba wamepelekwa hospitalini, baada ya kujeruhiwa vibaya, huku shughuli za uokoaji zikiendelea ili kuwaokoa wengine," ameongeza.


Kulingana na Abdullahi Baba Ara, madini kadhaa muhimu yanachimbwa katika eneo hilo kama vile dhahabu, tantalum na lithiamu. Idadi kamili ya wachimba migodi walionaswa haijafahamika mara moja, na waokoaji hawakuweza kufika eneo lililoporomoka kutokana na ukosefu wa usalama katika wilaya ya Shiroro.


"Tulipanga kwenda eneo hilo, lakini vikosi vya usalama vilituomba tusifanye hivyo kutokana na ukosefu wa usalama kutokana na kuwepo kwa makundi yenye silaha," ameeleza Abdullahi Baba Ara. Shiroro ni mojawapo ya wilaya kadhaa katika Jimbo la Niger zinazotishwa na makundi yenye silaha ambao hushambulia vijiji vilivyotengwa, kupora na kuchoma nyumba, na kuwateka nyara wakazi ili kuwalipa fidia.


Kwa sababu mbalimbali za kiusalama, serikali ya Jimbo la Niger imepiga marufuku uchimbaji madini katika wilaya za Shiroro, Munya na Rafi. Mamlaka katika jimbo hilo ina wasiwasi hasa kwamba rasilimali za madini zitahodhiwa na makundi yenye silaha. Lakini katika jimbo hili ambapo uchimbaji dhahabu ni mojawapo ya rasilimali pekee kwa wakazi, maeneo mengi ya uchimbaji madini yanaendelea kufanya kazi, licha ya onyo na marufuku.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii