Wafahamu wagombea wanaowania uchaguzi mkuu wa Julai 15 Rwanda

Nchini Rwanda, kinachosubiriwa sasa ni kuanza kwa kampeni kuelekea uchaguzi wa Julai 15 mwaka huu, baada ya mwishoni mwa juma wagombea 9 wakiwemo wagombea binafsi krejesha fomu zao kwa tume ya uchaguzi.

Wa kwanza ni Paul Kagame, rais wa sasa anayeomba kuchaguliwa tena kupitia chama cha RPF, ambaye anategemea uzoefu wake wa tangu mwaka 2000 kuwashawishi wananchi kumuamini.

Mwingine ni Frank Habineza, kiongozi wa chama cha DG, hili litakuwa ni jaribio jingine kwake baada ya kuanguka katika uchaguzi wa mwaka 2017, anasema yeye ana sera nzuri zitakazoibadili nchi hiyo.

Aidha yupo, Diane Shima Rwigara, anayewania nafasi hiyo kama mgombea huru, akijinasibu kuwa sera zake zimejikita katika kuikomboa nchi na kujenga uchumi wake.

Mwaka 2017 alizuiwa kugombea baada ya kushindwa kukusanya saini hitajika.

Wengine ni Herman Manirareba, anayewania kama mgombea huru, Innocent Hakizimana, yeye ni mwalimu wa shule ya msingi na anawania kama mgombea huru.


Wamo pia Thomas Habina, Fred Barafinda Sekikubo, Jean Mbanda na Philippe Mpayimana.Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii