Kura ya maoni ya kabla ya uchaguzi mkesha wa upigaji kura, mgombea wa chama tawala Claudia Sheinbaum, meya wa zamani wa mji wa Mexico na mwanasayansi aliyesomea fani hiyo, alikuwa anaongoza kwa asilimia 17 dhidi ya mpinzani wake mkuu wa chama cha upinzani, Xochitl Galvez.
Mgombea pekee mwanaume, wa mrengo wa kati Alvarez Maynez, alikuwa nyuma sana katika kura ya maoni.
Katika nchi yenye karibu Wakatoliki milioni 100, Sheinbaum atakuwa pia rais wa kwanza wa Mexico mwenye asili ya Kiyahudi, ingawa yeye sio mtu wa dini, kampeni yake ilisema.
Karibu watu milioni 100 walijiandikisha kupiga kura katika taifa hilo lenye watu wengi wanaozungumza Kispanish duniani, lenye wakazi zaidi ya milioni 129.
Katika taifa ambako siasa, uhalifu na ufisadi vinaingiliana, magenge ya kikatili yanayofanya biashara ya dawa za kulevya yametumia nguvu nyingi kuhakikisha wagombea wanaowataka wanashinda.
Saa chache kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza, mgombea kwenye uchaguzi wa mitaa aliuawa katika jimbo lenye machafuko la magharibi mwa nchi, maafisa wamesema, mmoja wa wanasiasa wengine 25 aliuawa wakati wa kampeni ya sasa, kulingana na takwimu rasmi.