Jamaa Aliyejaribu Kujirusha Kutoka Ghorofani Nairobi Apatikana Amefariki Chumbani Mwake

Wakaazi wa kijiji cha Pap Yamo huko Alego Magharibi wanaomboleza kifo cha ghafla cha mzee wa miaka 46. 

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwanamume huyo baada ya mwili wake kugunduliwa katika chumba chake cha kulala. Kulingana na Citizen Digital, mwanamume huyo aliyetambuliwa kwa jina Pascal Okoth Akelo alipatikana na jamaa zake. 


Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo alisema Elizabeth Awino kutoka kata ndogo ya Komenya aliripoti tukio hilo katika kituo cha Polisi cha Mwer. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii