Ama kweli Dunia ina mambo mengi ya kushangaza. Hebu mtazame huyo jamaa Pichani hapo chini.
Anaitwa Max More, yeye ni Bilionea Raia wa Kampuni ya Alcor Life Extension inayopatikana Jimbo la Arizona Nchini Marekani, ambayo ilianzisha mradi wa kuhifadhi miili ya watu waliofariki kwa kuiweka kwenye baridi kali ndani ya friji, wakitaraji kuja kuwafufua wafu hao ifikapo mwaka 2040 kwa kutumia teknolojia ambayo wamedai bado wanaifanyia utafiti.
Kampuni hiyo inamilikiwa na Bilionea Max More ambaye anasema alitumia miaka 12 kufanya kazi katika Wakfu wa Kampuni kongwe zaidi ya uchapishaji duniani, kwanza kama Mkurugenzi Mtendaji na kisha kama balozi na rais aliyestaafu, kabla ya kuachia ngazi na kuanzisha mradi wake huo ambao umeibua maswali mengi ya kisayansi, kisheria, kimaadili na kifalsafa.
Alcor imedai kuwa tayari ina miili 224 iliyohifadhiwa katika kituo chake cha hali ya juu huko Scottsdale, Arizona na ikiwa na Wanachama hai 1,418 waliojiandikisha kwa hiari yao na kusaini mikataba ya kuja kuhifadhiwa kituoni hapo baada ya kufa na kufufuliwa kipindi ambacho Teknolojia hiyo itakapoanza kufanya kazi.
Madai ya kuanzisha mradi huo, yaliibuka baada ya wenye Kampuni kudai Vitabu vya dini vinaelekeza kwamba mtu akifa, basi baadaye atakuja kufufuliwa na hivyo wao kama Alcor Life Extension wamegundua utaalamu huo na wataanza kuutumia utaalamu huo mwaka 2040 kwani kwasasa hakuna njia ya kufufua watu.