Siku tatu baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi ya muda ya uchaguzi wa urais wa Chad na ushindi katika duru ya kwanza ya rais wa mpito, Mahamat Idriss Déby, Waziri Mkuu Succès Masra, ambaye pia anadai ushindi, amewasilisha rufaa kwenye Baraza la Katiba.

Siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho, chama cha Les Transformateurs, ambacho kinapinga 18% ya kura kilizopata katika uchaguzi huo, kimewasilisha omalalamiko yake kwa Baraza la Katiba Jumapili usiku, anaripoti mwandishi wetu huko Ndjamena, Carol Valade. Chama cha Masra Success kinasema kilishinda uchaguzi wa urais kwa 73% ya kura, kulingana na hesabu yake, lakini bila kutoa maelezo.
Sitack Yombatina Béni, naibu kiongozi wa chama hicho, anabainisha idadi kubwa ya dosari wakati wa upigaji kura, hususan kukataliwa kuingia katika vituo vya kupigia kura au kushiriki katika shughuli za kuhesabu kura, ukosefu wa vifaa vya uchaguzi, masanduku ya kura yaliyochukuliwa na wanajeshi. Anaongeza kuwa aliwekwa mbali na mchakato na tume ya Taifa ya Uchaguzi, kinyume na kIbara ya 89 cha Maadili ya Uchaguzi.
Chama hiki pia kimeoliomba Baraza la Katiba, ili kupata maelezo ya matokeo ya uchaguei kituo kwa kituo chini ya kifungu cha 90 cha kanuni hiyo, ambacho kinasema: "Baraza la Katiba linatakiwa kutatatua tatizo ndani ya siku kumi baada ya kupokea malalamiko. Uamuzi wake unahusu utangazaji mahususi wa matokeo au kufutwa kwa uchaguzi.