P Diddy Ashtakiwa na Producer wake Kisa Kumladhimisha Kufanya Ngono na Makahaba
Msanii wa Marekani Sean Combs, maarufu kama P Diddy ameshtakiwa na mtayarishaji wa muziki ambaye anamtuhumu kwa kumshambulia kijinsia na kumlazimisha kufanya ngono na makahaba.
Mtayarishaji huyo, Rodney “Lil Rod” Jones ametuhumu kuwa alikuwa muathirika wa kutomaswa bila ridhaa wakati akifanya kazi ya utayarishaji wa albam mpya ya Diddy.
Haya ni mashtaka ya tano yenye tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya Bwana Combs.
Akijibu tuhuma hizo zilizowasilishwa katika mahakama ya jijini New York, mwanasheria wa Diddy amesema ni “uzushi mtupu.”
Wakili wa Bwana Combs, Shawn Holley, aliongeza kusema: “Tuna Ushahidi mkubwa na wa kutosha kuonesha madai yake hayo ni ya uongo.
“Tutajibu tuhuma hizi mahakamani na kuchukua hatua muafaka dhidi ya wanaofanya uzushi.”
Kwa mujimu wa nyaraka za mahakama, mtayarishaji huyo wa muziki aliishi na pia kusafiri na Bwana Combs kati ya Septemba 2022 na Novemba 2023.
Wanasheria wa Bwana Jones walisema alipewa dawa za kulevya na anakumbuka “kuamka akiwa uchi, ana kizunguzungu, na kuchanganyikiwa. Alikuwa kitandani na makahaba wawili na Bwana Combs”.
Bwana Jones pia anadai katika mashtaka yake kuwa Diddy alikuwa “akimtayarisha kwa ajili ya kumpeleka kwa rafiki zake” na amedai kuwa Diddy anajihusisha na “masuala ya uhalifu mkubwa”.
Picha kadhaa za sherehe za Bwana Combs zimejumuishwa kwenye mashtaka hayo. Nyaraka za mahakama zinadai kuwa picha hizo zinaonesha kuwepo na wasichana wenye umri mdogo na makahaba ambao mahakama inadai walipewa dawa za kulevya.
Bwana Jones anadai fidia ya dola milioni 30.
KÐ
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii