Mfahamu Mwanamke wa Mageuzi anayeinua Wakulima wa kahawa Kagera

Profesa Kokuletage Ngirwa,Aurelia Kamuzora  huyo ni Tanzania na ni miongoni mwanchi zinazotambulika kwa uzalishaji wa kahawa bora barani Afrika.

Miongoni mwa mikoa vinara katika zao hili ni kagera ,yenye historia ndefu ya kilimo cha kwanza tangu enzi za ukoloni. 

Hata hivyo,kwa muda mrefu wakulima wa mkoa huu wamekumbwa na changamoto kama bei duni,upungufu wapembejeo ,na ukosefu wa masoko ya uhakika.

Kupitia uteuzi wa profesa Aurelia kamuzora kuwa mwenyekiti wa Bodi ya kahawa Tanzania( TCB) hali hii inaanza kubadilika hatua kwa hatua.

Sababu za uteuzi wake: Uteuzi wa profesa Kamuzora haukuwa wa bahati nasibu .

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Daktari Samia Suluhu Hassan, alimteua kutokana na mambo makuu matatu:

* Uweledi na uzoefu wa kitaaluma.

* Uadilifu na udhubutu wa maamuzi.

* mtazamo wa maendeleo jumuishi.

Kupitia uongozi wake,Bodi ya kahawa imeanza kuleta mabadiliko yanayoguswa moja kwa moja na wakulima wa mkoa wa kagera,miongoni mwao ni haya.

1: Kuimarishwa kwa bei na masoko ya haki: Wakulima sasa wanapata bei bora zaidi kutokana na mfumo mpya wa mnada na mkataba ya moja kwa moja na wanunuzi,profesa kamuzora amesisitiza uwazi katika minada ili mkulima ajue thamani halisi ya zao lake.

2:Elimu ya kuongeza thamani ya kahawa.Wakulima wa kagera wameanza kupata mafunzo juu ya uchakataji bora wa kahawa ,kuanzia kuvuna hadi kukaanga ili kuongeza thamani kabla ya kuuza. 

Hii inawasaidia kupata faida zaidi kuliko hapo awali.

3: Upatikanaji wa miche na pembejeo bora : Bodi kwa sasa inashirikiana na taasisi za utafiti kuhakikisha miche bora isiyo athiriwa na magonjwa ,inawafikia wakulima kwa wakati .

Ikumbukwe kuwa Mkoa wa kagera ni miongoni mwavinuka wakuu wa mpango huu.

4: Uboreshaji wa miundombinu ya masoko na usafirishaji: Chini ya profesa kamuzora ,TCB inashirikiana na halmashauri za mikoa kuborsha vituo vya ukusanyaji kahawa ,kuhakikisha wakulima hawauzi kwa hasara au kupitia madalali wa kijanja( vishoka).

Akihojiana na mwandishi wa makala hii,Chief Miradi Syivester mfanyabiashara wa kahawa na mfugaji wilayani karagwe anasema tofauti kubwa inayojitokeza chini ya uongozi wake ni mtazamo wa kimaendeleo unaomweka mkulima mbele kama mdau mkuu na kama mtumishi wa mfumo.

Kwamba profesa kamuzora amehamasisha ushirikiano wa vikundi vya wakulima(cooperatives) na taasisi za kifedha ili wakulima wapate mikopo nafuu.

Pia ameanzisha mfumo wa kigitali uzalishaji wa mauzo ya kahawa ,jambo linalopunguza wizi na udanganyifu katika biashara ya kahawa.

Zaidi yayote Chief anaeleza kuwa amejenga uhusiano wa moja kwa moja kati ya wakulima,wanunuzi wa serikali.

Uongozi wa Prof. Aurelia kamuzora ni mfano wa jinsi elimu,maono na uzalendo vinavyoweza kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.

Kwa wakulima wa kagera huu niwakati wakutumia fursa, kuongeza uzalishaji na kulinda ubora wa zao lao.

Niwajibu wa kila mkulimakutambua kuwa maendeleo hayaji kwa bahati nasibu bali kwaushirikiano,uaminifu na juhudi.

Kama methali ya kiswahili isemayo"Aliyepanda kahawa kwa bidii atakunywa kwa furaha".

Mkutano wa Kampeini,wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu, Katika mkoa wa kagera umekuwa wa mafanikio makubwa sana kwa wingi wa wawatu ukichagizwa sana naongezeko la Bei ya kahawa,na juhudi zinazoendelea kuhakisha zao hili zilapanda thamani katika soko la dunia. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii