Kelvin Kiptum: Mahakama Yakataa Kusitisha Mazishi ya Mwanariadha Kufutia Kesi ya Baby Mama

Mahakama kuu imetupilia mbali ombi la kutaka kusitisha mazishi ya mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum. 


Mnamo Alhamisi, Februari 22, Ednar Owuor, kupitia kwa wakili wake Joseph Oyaro alifika kortini akitaka kuamuru kusitishwa kwa mazishi ya Kiptum. Katika maombi yake, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alidai kuwa alimzaa mtoto ambaye sasa ana mwaka mmoja na miezi saba na mshikilizi wa rekodi ya marehemu katika mbio za marathon. 


Owuor alifika kortini na mtoto huyo akitaka kusimamisha mazishi yaliyopangwa Ijumaa, Februari 23, akidai hawakumshirikisha katika mipango ya maziko. 


Kelvin Kiptum: Simanzi Huku Mwili wa Mshikilizi wa Rekodi ya Marathon Ukiondolewa Katika Makafani Read now ➤ Mwanzo Watu WATU Kelvin Kiptum: Mahakama Yakataa Kusitisha Mazishi ya Mwanariadha Kufutia Kesi ya Baby Mama Imewekwa upya Alhamisi, Februari 22, 2024 at 12:55 PM na  Shillah Mwadosho Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 alifikisha katika Mahakama Kuu mjini Eldoret Kutafuta maagizo ya kusitisha mazishi ya Kelvin Kiptum yaliyopangwa kufanyika Ijumaa, Februari 23 Katika ombi lake, mwanamke huyo alidai kuwa alizaa mtoto na Kiptum lakini familia yake inadaiwa haikumhusisha katika maandalizi ya mazishi Jaji Wananda alisema kuwa mipango ya mazishi iliendelea kwa muda huku gharama kubwa ikihusishwa MAKINIKA: Tusaidie kubadilisha maisha ya wengi, jiunge na programu ya Patreon kutoka TUKO.co.ke. Eldoret - Mahakama kuu imetupilia mbali ombi la kutaka kusitisha mazishi ya mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum. Msafara wa mwili wa Kelvin Kiptum mjini Eldoret. Picha: Lemar Ke. Chanzo: Twitter Mnamo Alhamisi, Februari 22, Ednar Owuor, kupitia kwa wakili wake Joseph Oyaro alifika kortini akitaka kuamuru kusitishwa kwa mazishi ya Kiptum. Katika maombi yake, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alidai kuwa alimzaa mtoto ambaye sasa ana mwaka mmoja na miezi saba na mshikilizi wa rekodi ya marehemu katika mbio za marathon. PIA SOMA Kelvin Kiptum: Simanzi Huku Mwili wa Mshikilizi wa Rekodi ya Marathon Ukiondolewa Katika Makafani Owuor alifika kortini na mtoto huyo akitaka kusimamisha mazishi yaliyopangwa Ijumaa, Februari 23, akidai hawakumshirikisha katika mipango ya maziko. MAKINIKA: Bofya “Ona Kwanza” chini ya “Fuatilia” ili kuona Habari za TUKO kwenye jukwaa lako la Habari Mwanamke huyo pia alitaka sampuli za DNA zichukuliwe kutoka kwa mwili ili kuthibitisha baba kabla ya mazishi kuendelea. Katika uamuzi wake, Jaji Wananda alikataa kutoa amri alizoomba mwanamke huyo. Wananda alisema kuwa mipango ya mazishi iliendelea kwa muda huku kukiwa na gharama kubwa, na itakuwa si haki kusitisha mazishi. "Mipango ya mazishi ya marehemu iko katika hatua ya kilele na kwa hivyo, kusimamisha mazishi kunaweza kutatiza hilo, kwa kuzingatia rasilimali ambazo zimewekwa," jaji aliamua. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii