Mgombea wa Upinzani aukaribia ushindi Senegal

Mgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, ambao ulifanyika baada ya miaka kadhaa ya ghasia na mzozo wa kisiasa.

Mshindi wa uchaguzi huo atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal, inayotazamwa kama kinara wa demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi, lililokumbwa na matukio ya mapinduzi, kuiondoa katika matatizo yake ya karibuni na kusimamia mapato kutoka kwa hifadhi za mafuta na gesi ambazo zinatarajiwa kuanza uzalishaji hivi karibuni.

Faye alikuwa amewaahidi wapiga kura mabadiliko makubwa na ya kweli na ameonekana kupata uongozi wa mapema dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa muungano unaotawala Amadou Ba.

Wagombea saba kati ya 17 wa urais wamempongeza Faye mwenye umri wa miaka 44 kutokana na dalili za mwanzo za kura nyingi alizopata zinazoendelea kuhesabiwa na kutangazwa kupitia vituo vya kuhesabia kura na yaliyochapishwa na vyombo vya Habari vya nchini humo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii