Ombeni amchinja mke wake, atenganisha kichwa

Simanzi na vilio vimetawala kwa wakazi wa kitongoji cha Masista kijiji cha Lusese Kata ya Igurusi baada ya Omben Kilawa mkazi wa kijiji hicho wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kumuua mke wake  Happness Mwinuka kwa kumchinja  na kutenganisha kichwa na Kiwiliwili.


Tukio hilo limetokea majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2024 ambapo jirani amesema alisikia kelele kama watu wanagombana lakini baada ya nusu saa kukawa kimya na kuamua kupiga yowe ndipo watu walipojitokeza na polisi kufika wamelibomoa mlango wa chumbani kwao na baada ya kuingia  Kilawa alikuwa ameshatekeleza mauaji kwa kumchinja mke wake na kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii