Ahukumiwa kifo kwa mauaji ya Monica

Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifo Joseph Kuria Irungu ‘Jowie’ kwa kuhusika na mauaji ya Mfanyabiashara Monica Kimani yaliyotokea Septemba 2018.

Hukumu hiyo, imetolewa na Jaji Grace Nzioka baada ya kutoa maelezo ya kina kuhusu kesi hiyo akisema kifungo cha nje kingewezekana endapo ikiwa Mshtakiwa angekiri shtaka na kuieleza Mahakama kwamba alikuwa tayari kubadilika kuwa mtu mzuri katika jamii.

Alisema, “ninaondoa uwezekano wa kifungo cha nje kwa mshtakiwa na kusalia na ama kifungo cha jela kwa muda, jela maisha, au kifo,” na kuongeza kuwa Mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa.

Josephanadaiwa kutekeleza mauaji hayo na kujipiga risasi begani kisha kutoa taarifa za uongo Polisi akidai alishambuliwa na majambazi katika lango la Royal Park Estate, Lang’ata jijini Nairobi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii