Mvua ya Kihonda Yaua Watu Wanne

Watu wanne wamefariki baada ya kusombwa na maji eneo la Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya mvua kubwa kunyesha leo January 25,2024.


Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amefika katika eneo la tukio usiku huu ambapo amesema hadi sasa wamepokea taariza za kuopolewa miili minne ya Watu waliofariki wakiwemo Wanaume watatu na Mwanamke mmoja.


“Hadi sasa Watu wanne taarifa zao zimeripotiwa kusombwa na maji mmoja amesombwa na pikipiki yake lakini nashukuru wote wamepaatikana hivyo tathmini kamili ntatoa kesho nikipata idadi kwa ujumla”


Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro Shabani Marugujo amesema hadi sasa wamefanikiwa kuokoa Familia 30 ambazo nyumba zao zilizingirwa na maji na kuwafikisha sehemu salama huku katika eneo hilo wakiopoa Watu wanne wakiwa wamefariki na zoezi linandelea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii