FAMILIA moja kutoka kijiji cha Ngeene, Kaunti ya Meru ilipata mshtuko baada ya kijana wa umri wa miaka 27 kuua mamake na nyanya, 90.
Wakazi walisema Jamleck Murithi alitekeleza unyama huo baada ya kuwatishia mara kadhaa.
Babake, Reuben Kabujo, alijaribu kuuzuia ukatili huo kwa muda wa saa moja bila kufanikiwa, mwanawe alipofika nyumbani akipiga kelele.
“Nilikuwa nimeketi chini ya mti nikinywa chai. Mwanangu alikuja na kuanza vurugu. Alinipiga ngumi akidai anakuja kunimaliza,” alisema Bw Kabujo.