RC CHALAMILA ATOA UFAFANUZI WA UHABA WA SUKARI NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 19, 2024 akiwa katika Mkutano wa hadhara Wilaya Temeke Jimbo la Mbagala ametoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya uhaba wa Sukari hapa nchini na jitahada za Serikali Chini ya kiongozi mahiri Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na Changamoto hiyo.

RC Chalamila amesema si kweli hata kidogo kuwa Serikali haina majibu kuhusu uhaba wa Sukari pia sio sahihi kuwa Sukari haipatikani kwa sababu kuna wafanyabishara wameficha, ukweli ni kwamba katika Kipindi cha mwezi wa kumi na moja, kumi na mbili mwaka jana na mwezi wa kwanza mwaka huu viwanda vya ndani havikufanya uzalishaji wa Sukari

Sababu kubwa ya viwanda kutofanya uzalishaji hususani kiwanda cha Kilombero, mtibwa, kiwanda cha Moshi, Bagamoyo na Dakawa ni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika mashamba ya miwa maji yalijaa na barabara ziliharibika kwa kiasi kikubwa ambapo hakuna magari yaliyoweza kuingia kwenye mashamba hayo.

Hivyo kutokana na kadhia hiyo uzalisha wa Sukari ulikuwa hafifu kwa kuwa miwa ikiwa katika hali nzuri tani 10 huweza kuzalisha Sukari tani 1 na miwa iliyoko kwenye maji tani 18 huweza kuzalisha Sukari tani 1.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii