Kura ya kuahirisha uchaguzi yafutwa Senegal

Baraza la Katiba la Senegal, limebatilisha tangazo la kuchelewesha uchaguzi wa rais, uliokuwa ufanyike mwezi huu likisema kura ya Bunge ilikuwa kinyume na katiba likidai muswada uliopitishwa ulikuwa kinyume na katiba.

Awali, ni baraza hilo pia lilibatilisha agizo la Rais Macky Sall la Februari 3, 2024 ambalo lilirekebisha kalenda ya uchaguzi wiki tatu kabla ya kupiga kura ambapo Rais Macky Sall mapema mwezi huu alitoa tangazo la kuchelewesha uchaguzi ambao ulikuwa ufanyike Februari 25, 2024.

Uamuzi huo, uliitumbukiza Senegal katika mzozo mbaya wa kisiasa na kuchochea hasiara kubwa ya umma na maandamano ya vurugu na vikosi vya usalama vilivamia majengo ya bunge na kuwaondoa baadhi ya wabunge wa upinzani waliokuwa wakipinga muswada.

Kura hiyo ilikuwa ikimpa njia kwa rais Sall, ambaye mamlaka yake ya muhula wa pili yanatarajiwa kumalizika mwezi Aprili 2024, kuweza kusalia mamlakani hadi mrithi wake atakapopatikana na sasa hali imekuwa tofauti.

Hata hivyo, VYnama vya Upinzani na makundi ya asasi za kiraia yameitisha maandamano mapya leo Ijumaa. Maandamano mengine ya amani yaliyoandaliwa na jumuiya ya asasi za kiraia yamepangwa kufanyika Jumamosi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii