Wanachi kulindwa siku ya sikukuu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama linaendelea kuimarisha ulinzi ambapo limebainisha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya litahakikisha sikukuu hizo zinasherekewa kwa amani na utulivu hasa ikizingatiwa kuwa mkoa huo ni kitovu cha utalii hapa nchini.


Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo, amesema katika kuhakikisha sikukuu hizo zinasherehekewa kwa amani na utulivu Jeshi hilo litahakikisha linatoa ulinzi kwenye nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na maeneo mengine yote ambapo Askari watapangwa katika doria za miguu, pikipiki, magari na doria za mbwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii