UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUWA WA KIMATAIFA

SERIKALI INATARAJIA KUANZA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA JIJINI MWANZA NA KUWA NA HADHI YA KIMATAIFA

HAYO YAMEBAINISHWA NA MKUU WA MKOA HUO CPA AMOS MAKALLA AMBAPO AMESEMA KUWA UJENZI HUO UTAANZA NA JENGO LA ABIRIA NA TAYARI MKANDARASI AMESHAPATIKANA AMBAPO UKENZI HUO UTAANZA RASMI MWEZI WA PILI MWA KA HUU.

MH MAKALLA AMESEMA KUWA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA UWANJA HUO KUTASAIDIA USAFIRISHAJI WA MINOFU YA SAMAKI KUTOKA JIJINI MWANZA KWENDA NCHI MBALIMBALI BADALA YA KUTUMIA UWANJA WA NDEGE WA ENTEBE NCHINI UGANDA.

 MKUU WA MKOA HUO AMEELEZEA MIKAKATI ILIYOPO ITAKAYOIFIKISHA MWANZA KATIKA UCHUMI MKUBWA KUPITIA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOFANYWA NA WAKAZI WA JIJI HILO ZIKIWEMO ZA KILIMO, UVUVI NA MADINI AMBAVYO VINACHANGIA ASILIMIA 7.7 PATO LA TAIFA NA KUIFANYA MWANZA KUWA MKOA WA PILI KATIKA KUCHANGIA ONGEZEKO KATIKA  PATO LA TAIFA.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii