Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema nchi yake itaendelea kufanya biashara na mataifa ya kigeni ambayo hayatakuwa yanaingilia uhuru wake, matamshi aliyoyatoa majuma kadhaa tangu Marekani iiondoe nchi yake katika mkataba wa kibiashara AGOA.
Tangu atie saini sharia tata kuhusu ushoga, rais Museveni amekuwa katika shinikizo kutoka kwa mataifa ya magharibi yanayotaka abatilishe sharia hiyo, ambayo wanasema inakiuka haki za binadamu.
Marekani ilitishia kwa mara ya kwanza kuiwekea vikwazo Uganda na kuiondoa kutoka kwa mkataba wa biashara wa AGOA mwezi Mei, baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupitisha sheria yenye utata dhidi ya ushoga.
Sheria inatoa adhabu ya kifo kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.