Mashambulizi ya Israel ukanda wa Gaza yamewauwa watu 73

Wapalestina 73 wameuwawa na wengine 99 wamejeruhiwa katika muda wa saa 24 zilizopita kutokana na mashambulizi ya vikosi vya Israel yanayoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.


Hayo yameelezwa na wizara ya afya ya Ukanda huo inayoongozwa na kundi la Hamas.

Kwa upande wake jeshi la Israel limesema limewauwa wapiganaji 10 wa kipalestina kusini mwa Gaza katika operesheni iliyofanikiwa kuharibu ghala moja la silaha na kugundua moja ya mahandaki ya maficho.

Wakati huo huo ndege na helikopta za Israel zimefanya mashambulizi nchini Lebanon dhidi ya maeneo ambayo jeshi la nchi hiyo linasema yanatumiwa na kundi la Hezbollah.


Hayo yakijiri mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani na Marekani wanaitembelea Mashariki ya Kati kwa mara nyingine kujaribu kutuliza mivutano inayotishia kuutanua mzozo wa Gaza.

Mwanadiplomasia wa Ujerumani Annalena Baerbock anaelekea mjini Ramallah huko Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na viongozi wa Palestina baada ya kufanya mashauriano na viongozi wa Israel mjini Tel Aviv.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii