Mwanaume mmoja amemshambulia jaji wakati hukumu yake katika chumba cha mahakama cha Nevada, Marekani ikisomwa siku ya Jumatano.
Tukio hilo lililonaswa katika kamera za CCTV – linamuonyesha Deobra Redden, 30, akirukia meza ya jaji na kumshambulia kabla ya wafanya kazi wa mahakama kuingilia kati.
Alikuwa mahakamani kusikiliza hukumu baada ya kupatikana na hatia ya kushambulia na kusababisha majeraha, msemaji wa Mahakama ya Wilaya alisema.
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji, Jaji Mary Kay Holthus “alipata majeraha kidogo” baada ya kuanguka katika kiti chake. Wasaidizi wa mahakama walimsaidia na kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu.
Kabla ya Redden kuruka juu ya benchi, wakili wake alimwomba Jaji Holthus amhukumu Redden kipindi cha uangalizi.
Nadhani ni wakati wa yeye kupata ladha ya kitu kingine,” Jaji Holthus alisema na kufuatiwa na shambulizi la Rudden.I
dara ya Polisi ya Metropolitan ya Las Vegas ilisema wapelelezi wanachunguza tukio hilo la mahakamani.