Waliojaribu mapinduzi Sierra Leone wafunguliwa mashitaka ya uhaini

Sierra Leone, Jumanne imewafungulia mashitaka ya uhaini watu 12, na makosa mengine kwa ushiriki wao wa kile serekali imekiita jaribio la mapinduzi Novemba 26, imesema taarifa kwa vyombo vya habari.

Kati ya wale walio shitakiwa ni Amadu Koita, ambaye serekali imesema alikuwa mmoja wa waliopanga jaribio la mapinduzi.

Mwanajeshi na mlinzi wa rais wa zamani Ernest Bai Koroma, Koita kwa kiwango kikubwa alikuwa na wafuasi katika mitandao ya kijamii ambapo amekuwa akiikosoa serekali ya sasa ya rais Julius Maada Bio.

Alikamatwa Desemba 4, na ni mmoja wa watu 85, wengi wao ni wanajeshi ambao walikamatwa wakihusishwa na matukio ya Novemba 26.

Watu hao 12 wanaohusishwa wanajumuisha maafisa wa zamani wa polisi walifunguliwa mashtaka ikijumuisha ya uhaini, kutaka kufanya uhaini, njama, kusaidia, na kushirikiana na adui kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na waziri wa habari Chermor Bah.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii