Mama mbaroni kwa kumuua mwanaye kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji

Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Johari Mbuma (19), mkazi wa Kigamboni Manispaa ya Iringa anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake mwenye umri wa miezi saba kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji chooni kichwa chini miguu juu akiwa Mtaa wa Mawelewele.


Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Novemba 21, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, akisema uchunguzi unaendelea.


Video ambayo Mwananchi imeiona, inamwonyesha Johari akieleza tukio hilo baada ya kukamatwa na Polisi, akisema alitoka kwao na kwenda kwa rafiki yake na baadaye alipobanwa haja aliingia chooni ambako baada ya kumaliza, alimtumbukiza mtoto kwenye ndoo nyeupe iliyokuwa na maji.


Mwenyekiti wa mtaa wa Mawelewele, Obedi Mtatifikolo amesema alipata taarifa Jumapili, Novemba 19, 2021 na alitoa taarifa polisi ambao walifika kuchukua mwili wa mtoto huyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii