Kaunti ya Mombasa pwani ya taifa hilo na Tana River huko kaskazini Mashariki ni baadhi ya majimbo yalioathirika.
Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema familia 156 katika eneo la Bandi huko Garsen katika kaunti ya Tana River Kaskazini Mashariki wamehama makazi yao baada ya nyumba zao kufurika, idadi hiyo ikihofiwa kuwa huenda ikaongezeka.
Kwa mujibu wa baadhi ya video zilizosambazwa na shirika hilo la vyombo vya habari vya ndani, baadhi ya makaazi ya watu yamejaa maji haswa katika kaunti ya Mombasa.
Ripoti kutoka kwa shirika la msalaba mwekundu zinaeleza kuwa watu 52 wamefariki kutokana na mafuriko wakati huu wengine 24,415 wakiwa wamepoteza makazi yao katika maeneo tofauti ya nchi.