Mwili waokotwa ukiwa umeuawa Mwanza

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 hadi 18, amekutwa amefariki eneo la Dampo kata ya Buhongwa Mwanza kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wa wanaeleza kuwa kijana huyo alikuwa anaishi na wenzake wanne kwenye chumba kimoja japo bado hawajafahamu kwa kina hasa kilichomsibu hadi umauti kumkuta.


Balozi wa mtaa wa Shibai kata Buhongwa Deo Melikyadi, amesema kijana huyo aliyemtambulisha kwa jina moja la Ally, alikutwa amefariki leo asubuhi majira saa 11 alfajiri ambapo alikuwa amechomwa na kitu kinachosadikika kuwa kisu maeneo ya tumboni na shingoni.


"Baada ya kufika kwenye tukio nikamkuta huyu mtu aliyechomwa kisu anaitwa Ally, ndipo ikamtafuta mwenyekiti wa mtaa akaja na wajumbe tukamuangalia tukagundua kweli Ally amechomwa kisu tumboni na shingoni, alikuwa anakaa kwenye chumba cha kupanga na wenzake wanne tumewauliza wanasema hawajui ilikuwaje' amesema mjumbe.


Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeuchukua mwili wa kijana huyo kwa ajili ya uchunguzi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii