Iran imeimarisha uwezo wake wa ulinzi wa anga kwa kuongeza ndege zisizo na rubani zilizo na makombora ya angani kwa silaha zake, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Jumapili.
Darzeni ya ndege zisizo na rubani za Karrar zilizojihami kwa makombora ya angani zimeongezwa kwa ajili ya ulinzi wa anga katika maeneo yote ya mipaka ya nchi, shirika la habari la IRNA limesema.
Ndege hizo zisizo na rubani, zenye uwezo wa kufanya kazi kwa umbali wa hadi kilomita 1,000 zilionyeshwa Jumapili asubuhi kwa saa za huko wakati wa sherehe iliyoonyeshwa kwenye televisheni iliyoandaliwa kwenye chuo cha kijeshi mjini Tehran.
"Maadui sasa watalazimika kufikiria upya mikakati yao, kwa sababu vikosi vya Iran vimeimarisha nguvu zaidi", IRNA ilimnukuu kamanda mkuu wa jeshi la Iran, Jenerali Abdolrahim Mousavi, akisema.