Jeshi la Israel ladai kuuzingira mji wa Khan Younes, kusini mwa Gaza

Mapigano makali yanaendelea Alhamisi, Desemba 7, katika Ukanda wa Gaza kati ya Hamas na jeshi la Israel, ambalo liliuchukua mji mkubwa wa Khan Younes ambapo inamsaka mtu inayemdhania kuwa ndiye aliyepanga shambulio la umwagaji damu Oktoba 7.

Msemaji wa jeshi la Israel kwa Kiarabu amechapisha taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ikiitwa Twitter) ikibaini kwamba kwamba mapigano katika jimbo la Khan Younes  haruhusu shughuli au kutembea kwa raia kwenye barabara ya Salah Al Dine ambayo imekuwa "uwanja wa vita". Wakati wa awamu ya kwanza ya mapigano hayo, ni kupitia njia hiyo ambapo raia walihimizwa kufika kusini mwa Ukanda wa Gaza, wakidaiwa kuwa salama kutokana na mapigano.

"Jeshi la Israeli litaidhinisha shughuli za kibinadamu za raia kupitia barbara ilioko magharibi mwa Khan Younes," linabainisha kati ya mambo mengine arifa, ambayo ramani imeambatishwa. Usafiri kutoka eneo la Rafah na Khan Younes hadi Deir Al-Balah na kambi za kati utawezekana kupitia njia zifuatazo: Mtaa wa Al-Rashid "Al-Bahr" na Mtaa wa Al-Shuhadaa huko Deir Al-Balah.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii