Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Yatinga WAFCON

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imefuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa upande wa soka la Wanawake WAFCON 2024 baada ya ushindi wa jumla wa magoli 3-2 dhidi ya Togo.

Twiga Stars ilipata ushindi wa magoli 3-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani [Tanzania] kabla ya leo kupoteza ugenini [Togo] kwa kufungwa 2-0.

Twiga Stars imefuzu WAFCON 2024 ikiwa ni siku chache baada ya Taifa Stars pia kufuzu AFCON 2023. Kwa mara ya kwanza Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye mashindano makubwa ya soka barani Afrika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii