Watu 120 wamekufa kwa mafuriko nchini Kenya

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko yaliyokumba maeneo kadhaa nchini Kenya imefikia 120 huku maelfu ya makaazi yamesombwa na maji na kuwalazimisha watu kutafuta hifadhi.


Takwimu hizo mpya zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya, Raymond Omollo, ambaye pia amesema kaunti 4 za upande wa mashariki mwa nchi hiyo ndiyo zimeathirika zaidi na nyingine 10 zimo kwenye hali ya juu ya tahadhari.

Kulingana na afisa huyo, jumla ya nyumba 89,000 zimeharibiwa kwa mafuriko, hali iliyoilazimisha serikali kuanzisha kambi 112 za kuwahifadhi wale walipoteza maakaazi.

Rais William Ruto aliongoza kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri kujadili athari za mafuriko na kuahidi kutoa mabilioni ya shilingi za Kenya kuwasaidia waliokumbwa na maafa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii