Afisa katika chama cha upinzani DRC ameuawa na makundi hasimu ya kisiasa

Ghasia hizo zilimuua Dido Kasingi, wakili na baba wa watoto sita ambaye alikuwa rais wa vijana katika chama cha Katumbi, “Together for the Republic”, msemaji wa chama hicho aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa.

Afisa mmoja wa chama cha upinzani aliuawa Jumanne wakati wa mapigano kati ya makundi hasimu ya kisiasa katika eneo tete la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyanzo vimesema.

Taifa hilo maskini la Afrika ya kati lenye watu milioni 100 linafanya uchaguzi wa wabunge na rais hapo Desemba 20, huku kampeni zikiwa zimeanza siku tisa zilizopita.

Mapigano ya Jumanne yalizuka wakati msafara wa kampeni wa mgombea urais wa upinzani Moise Katumbi ulipopita Kindu, mji mkuu wa jimbo la mashariki ya Maniema. Mashuhuda wanasema wafuasi wa Katumbi walipigana na wafuasi wa chama tawala cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS) cha Rais Felix Tshisekedi.

Ghasia hizo zilimuua Dido Kasingi, wakili na baba wa watoto sita ambaye alikuwa rais wa vijana katika chama cha Katumbi, “Together for the Republic”, msemaji wa chama hicho aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa. Msemaji wa chama cha upinzani Herve Diakiese, alimshutumu gavana wa Maniema kwa kuchochea ghasia hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii