Mrembo wa Kenya aliyechora tattoo ya Harmonize amfuata Tanzania

Mwanadada mmoja mzaliwa wa Kenya aliyejitabulisha kwa jina Catherine almaarufu 'Kutu' Mkenya, amefunguka wazi na kusimulia upendo wake kwa msanii kutokea Tanzania Harmonize baada ya kuchora Tattoo zake mwilini mwake.


Kulingana na mwadada huyu kuchora tattoo za msanii Harmonize mwilini mwake ikiwemo mgongoni ,kifuani na hata miguuni kulichangiwa na hisia zake za upendo kwa msanii huyo jambo ambalo lilimfanya kufunga safari hadi Tanzania Kumtafuta.


"Nilitumia pesa nyingi sana ili kuchora tatoo ya Harmonize mwilini mwangu nilifanya hivyo kwa upendo wangu kwake, nampenda sana kila siku namuwaza, ndipo niliamua kufunga safari yangu hadi Tanzania lengo langu kuu ikiwa ni kuonana na Harmonize ili niweze kumueleza upendo wangu kwake,"alisema.


Mwanadada huyo ambaye alifanyiwa mahojiano na wanablogu nchi Tanzania alisimulia kuwa wengi walimkejeli kwa kuchora tattoo za mwanaume mwilini kwake ila kulingana naye ni jambo la kujivunia kwa kuwa alitumai kuwa siku moja Harmonize atapedezwa na jambo hilo.


"Watu wengi hawakupedezwa na tattoo zangu zenye maandishi 'Konde na Harmonize' mwilini ila kwangu najivunia kuwa nazo kwa kuwa ninampenda Harmonize na roho yangu yote kila mmoja ana huru wa kufanya jambo lolote upendalo duniani," alisema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii