WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watanzania kushirikiana na kushikamana ili kuyapa thamani madini ya Tanzanite na kuifanya dunia nzima itambue kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu na tayari imeweka mazingira ya kuyaongezea thamani.
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 26, 2022) alipozungumza na wananchi katika eneo la EPZA unapojengwa Mji wa Tanzanie katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kukutana na wafanyabiashara wa sekta madini kwa lengo la kuhakikisha kwa pamoja wanaweka mikakati ya kusaidia kuikuza sekta hiyo ili iendelee kuleta tija kwa watanzania na taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Majaliwa aliwasisitiza wananchi waendelee kufanya biashara hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla na kwamba Serikali ipo tayari kuwahudumia wakati wote. “Tumejipanga kuwahudumia iwe wakati wa jua au wakati wa mvua.