Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua watu 558 huko Gaza

Mashambulizi ya anga ya Israel yameua zaidi ya watu 558 katika Ukanda wa Gaza, Wizara ya Afya katika eneo la Palestina imesema.Zaidi ya watu 65 zaidi wamehesabiwa kuwa wamekufa, na kuongeza jumla ya waliouawa, huku zaidi ya 2,800 wamejeruhiwa.Israel ilianzisha mashambulizi hayo baada ya shambulio kubwa la shirika la Palestina la Hamas, linalotawala Ukanda wa Gaza.Takriban watu 700 wameuawa nchini Israel na wengine karibu 2,400 kujeruhiwa katika umwagaji damu mbaya zaidi wa raia katika historia ya Israel.Zaidi ya Waisraeli 100 pia wamechukuliwa mateka katika Ukanda wa Gaza. na Hamas inasema mateka wanne waliuawa na mashambulizi ya anga ya Israel.

Hamas imeorodheshwa kama shirika la kigaidi na Umoja wa Ulaya, Marekani na Israel.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii