Licha
ya mlipuko wa virusi vya corona, watu matajiri barani Afrika wameongeza
utajiri wao zaidi ya walivyokuwa miaka minane iliopita.
Mabilionea
wa bara hili kwa jumla walijipatia $84.9 bilioni ikiwa ni asilimia 15
zaidi ya utajiri wao miezi 12 iliopita na kwamba ni dadi kubwa
iliyojumlishwa tangu 2014 ambapo kulikuwa na mabilionea 28 kulingana na
jarida la Forbes.
Jarida la Forbes lilitumia bei za hisa na thamani ya ubadilishanaji wa fedha kuanzia Januari 19 2022 ili kupima utajiri wao.
Afrika
Kusini na Misri ndio mataifa yenye mabilionea wengi, nchi zote mbili
zikiwa na mabilionea watano kila mmoja zikifuatiwa na Nigeria yenye
mabilionea watatu huku Tanzania ikiwa na bilionea mmoja ambaye ni
mfanyabiashara Mohammed Dewji.