Shabiki Mwingine Wa Yanga Auawa Geita Na Walinzi

Mfanyabiashara mmoja ambaye pia alikuwa Shabiki wa Yanga, Alex Mayaya (40), mkazi wa Mji mdogo wa Katoro, Geita ameuawa kwa kupigwa rungu na walinzi wa Kampuni ya Samike Security Company akidhaniwa kuwa ni mwizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa Novemba 5, 2023 ambapo inaelezwa kuwa marehemu alikunywa kiwango kikubwa cha pombe akisherehekea ushindi wa timu yake, kabla ya kwenda dukani kwake usiku na kufungua.

Kamanda Jongo amesema kuwa marehemu alitoa matairi mawili ya pikipiki dukani kwake, ambapo kwa kuwa duka hilo lilikuwa likiendeshwa na kijana wake, walinzi hawakuwa wakimjua na kudhani kwamba ni mwizi, kabla ya kujichukulia sheria mkononi na kumpiga na rungu.

Ameeleza kuwa jeshi hilo linawashikilia walinzi watatu kwa tuhuma za kutekeleza mauaji hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii