Umoja wa Mataifa unasema muda unapita wa kuzuia janga la kibinadamu Gaza kutokea

Ujumbe wa waatalamu wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa pamoja na mfuatiliaji maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yanayokaliwa ya Wapalestina Francesca Albanese, umesema Alhamisi kwamba muda unapita kuweza kuzuia mauwaji ya kimbari na janga la kibinadamu kutokea huko Gaza.

Israel inasema matamshi hayo ni propaganda ya kundi la Hamas.

Katika taarifa ya pamoja waatalamu hao wanasema wana imani kwamba watu wa Palestina wako katika hatari kubwa ya mauwaji ya kimbari.

Wameongeza kusema kwamba washirika wa Israel pia wanabeba mzigo wa kuwajibika na ni lazima wachukuwe hatua za haraka na dharura sasa hivi kuzuia janga hilo kukamilika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii