Uganda yamkamata mkuu wa wanamgambo anayetuhumiwa kwa mauaji

Uganda ilisema Alhamisi kuwa imemkamata mkuu wa kikosi cha wanamgambo wanaolaumiwa kwa mauaji ya watalii wawili wa kigeni waliokuwa wakienda honeymoon na kiongozi wao wa ndani katika mbuga ya wanyama mwezi uliopita.

Alikuwa ni mtu pekee aliyenusurika katika oparesheni ya usiku ya kijeshi Jumanne dhidi ya kikosi cha wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) ambacho kiliwaua wapiganaji wengine sita, jeshi lilisema.

Muingereza na Mwafrika Kusini waliuawa pamoja na kiongozi wao katika shambulio la Oktoba 17 walipokuwa safarini katika Mbuga ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth.

Uganda ililaumu ADF, wanamgambo wenye silaha wenye makazi yao katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao wanashirikiana na kundi la Islamic State (IS).

"Hii ilikuwa operesheni yenye mafanikio ya kijeshi iliyoongozwa na kijasusi na kikosi kizima ambacho kilikuwa kimetumwa na ADF kusababisha ghasia, kuua watalii, kuchoma shule, hospitali, kiliondolewa," Akiiki alisema.

"Mtu pekee aliyenusurika ni kamanda tuliyemkamata," alisema, na kuongeza kwamba sasa atakabiliwa na kesi.

Akiiki alisema Njovu alikutwa na baadhi ya mali za watalii waliouawa na kitambulisho cha kiongozi wao wa Uganda.

Meja Jenerali Dick Olum, anayesimamia operesheni za kijeshi za Uganda dhidi ya ADF nchini DRC, alisema wanachama wengine sita wa kikosi hicho waliuawa kwa kupigwa risasi katika operesheni ya Jumanne.

Waathiriwa wa shambulio la Oktoba wametajwa kuwa ni raia wa Uingereza David Barlow, mke wake wa Afrika Kusini Celia na muongozaji, Eric Ayai.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii