Mbunge Atekwa na Wasiojulikana, Akutwa Mtupu

Mbunge wa Chama cha Upinzani cha Citizens Coalition for Change – CCC, nchini Zimbabwe, Takudzwa Ngadziore (25), anadaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana na kisha kutupwa takriban kilomita 50 kaskazini mwa mji mkuu wa Taifa hilo, Harare.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, Mbunge huyo kijana kabla ya tukio la kutekwa aliweka video mubashara kwenye mtandao wa Facebook, akionesha mwanamme akikimbia kuelekea alipo akiwa ameshika Bunduki aina ya Riffle, kabla ya video hiyo kukatizwa ghafla baada ya sekunde saba.


Wafuasi wa CCC cha Nelson Chamisa. Picha ya Bulawayo 24.
Hata hivyo, alipatikana karibu na migodi iliyopo kwenye kijiji cha Mazowe, akiwa amechapwa vibaya na kuachwa mtupu, huku ikidaiwa alichomwa kwa sindano yenye kemikali isiyojulikana.

Kinara wa chama chake bungeni Amos Chibaya na Msemaji wa CCC, Promise Mkwananzi walithibitisha tukio hilo, wakisema kwamba watawasilisha ripoti kwa polisi, kama hatua za awali za kulaani tukio hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii