Watu zaidi ya 70 hawajulikani walipo baada ya kutokea ajali ya boti

Nchini Nigeria, zaidi ya watu 70 hawajulikani walipo, kufuatia ajali ya boti iliotokea mwishoni mwa juma lililopita katika jimbo la tabara kaskazini mwa nchi hiyo.

Wafanyakazi wa uokoaji nchini humo wameendeleza shughuli za kuwatafuta watu hao takriban 73, ambao hadi sasa hawajulikani walipo.

Kulingana na mamlaka, boti hilo lililokuwa limewabeba watu 104 kutoka jimbo hilo lilizama katika mto mmoja siku ya jumamosi, miili 18 ikipatikana baada ya ajali hiyo.

Usafiri wa majini ni wakawaidia nchini humo, lakini mara nyingi ajali za boti hutokea kutokana na kupakia kupita kiasi, na ukosefu wa uangalizi hasa katika kipindi cha mvua.

Mapema mwezi huu, watu 40 walitoweka baada ya boti lililokuwa na watu 50 kuzama katika jimbo la Kebbi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii