Baada ya kufanikiwa kufunga ‘Hat Trick’ dhidi ya Azam FC Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans, Stephane Azizi Ki ameyachambua mabao yake hayo matatu.

Aziz Ki amesema kuwa anashindwa kuchagua lipi ni bao zuri kati ya yale yote matatu ambayo amefunga dhidi ya Azam FC kwa kuwa anaamini kila bao lilikuwa na mchango wake katika mchezo.

Azizi Ki baada ya kufunga mabao hayo sasa anakuwa kinara wa upachikaji mabao ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa nayo sita huku akifuatiwa na Jean Baleke wa Simba SC ambaye amefunga matano.

Juzi Jumatatu (Oktoba 23) Young Africans ilikuwa dimba la nyumbani Benjamin Mkapa na kufanikiwa kuichapa Azam FC mabao 3-2 na hivyo kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 15. huo.


“Kwanza nipende kuwashukuru mashabiki wa Young Africans kwa kutupa sapoti kubwa katika mchezo huu mpaka tumefanikiwa kupata matokeo ni jitihada zao ambazo zilitufanya kupambana mpaka tukapata ushindi.


“Kuhusu lipi ni bao langu bora kati ya yale matatu ambayo nilifunga niseme tu kuwa yote yalikuwa mabao mazuri, lakini lile la kwanza lilikuwa zuri kwa kuwa wengi hawakutarajia kama ningeweza kufunga katika mazingira yale.