Urusi imeishtumu Ukraine kwa kujaribu kushambulia makazi ya Rais Vladimir Putin na kuapa kulipiza kisasi, bila kutoa ushahidi wa madai hayo ambayo Ukraine imeyapuuza na kuyataja kutokuwa na msingi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Ukraine ilijaribu kushambulia makazi ya Putin katika mkoa wa Novgorod magharibi mwa Moscow mnamo Desemba 28-29 kwa droni 91 za masafa marefu ambazo zote zilidunguliwa na ulinzi wa anga wa Urusi.
Katika taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Urusi, Lavrov amesema hakuna aliyejeruhiwa na hakukuwa na uharibifu wowote.
Hata hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha kwa njia huru taarifa hiyo ya Lavrov. Pia haikubainika wazi alipokuwa Putin wakati wa shambulizi hilo.
Kwa upande wake, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Putin alimuelezea kuhusu shambulizi hilo kwa njia ya simu, hali iliyomghadhabisha. Hata hivyo amesisistiza matumaini yake ya kupatikana kwa makubaliano ya amani hivi karibuni.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii