Helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Kenya imeanguka Lamu, na kuua idadi ambayo bado haijafichuliwa ya wahudumu na wanajeshi waliokuwa katika ndege hiyo.
Taarifa kutoka kwa KDF mnamo Jumanne, Septemba 19, ilionyesha kuwa helikopta ya Kenya Air Force Huey ilianguka Jumatatu usiku.
KDF ilisema wafanyakazi na wanajeshi waliokuwa ndani ya chopa hiyo walikuwa wakifanya oparesheni ya angani inayoendelea ya amani Boni. "Uongozi na jumuiya nzima ya KDF inawapa pole familia za wafanyakazi hao. Bodi ya uchunguzi imeundwa na kutumwa katika eneo la tukio ili kubaini chanzo cha ajali," taarifa hiyo ilisema.