Meya na maafisa watano wafukuzwa kwa vifo vya watu 107 Iraq.

Mamlaka nchini Iraq imesema meya na mkuu wake wa zimamoto ni miongoni mwa maafisa watano wa taifa hilo waliofutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa uzembe mkubwa baada ya ajali ya moto iliyoua watu 107.

JAMIIIRAQ

Meya na maafisa watano wafukuzwa kwa vifo vya watu 107 Iraq.

Sudi Mnette
Dakika 59 zilizopita

Mamlaka nchini Iraq imesema meya na mkuu wake wa zimamoto ni miongoni mwa maafisa watano wa taifa hilo waliofutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa uzembe mkubwa baada ya ajali ya moto iliyoua watu 107.

https://p.dw.com/p/4X1oa
Vikosi vya uokozi vikiwa nje ya hospitali ya Hamdaniyah ambako majeruhi wa ajali ya moto kwenye harusi nchini Iraq Septemba 27, 2023 walipelekwa
Picha: ZAID AL-OBEIDI/AFP/Getty Images

Mamlaka nchini Iraq imesema meya na mkuu wake wa zimamoto ni miongoni mwa maafisa watano wa taifa hilo waliofutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa "uzembe mkubwa" baada ya ajali ya moto ya wiki iliyopita ulioua watu 107 kwenye harusi.

Duru zinaeleza pamoja na kushtakiwa kwa uzembe meya huyo atashitakiwa kwa kuruhusu ujenzi holela wa jengo kulikotokea maafa hayo.

Mkasa huo ulitokea katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Qaraqosh, sehemu ya jamii ndogo ya Wakristo wa Iraq karibu na Mosul, katika ukumbi wa harusi uliokuwa na uwezo wa kuchukua takriban watu 400.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii