Polisi wameanzisha uchunguzi katika kisa ambacho mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 55, amefariki katika chumba cha hoteli nchini Kenya, baada ya kufurahia burudani ya tendo la ndoa kati yake na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25.
kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya ndiwa,poul riyoba amesema kisa hicho kimetokea usiku wa ijumaa januari 21 na mwanaume ambae jina lake haliwezi kutajwa kwa sababu alikua afisa wa polisi.
mwanaume huyo ameripotiwa kuzimia na kufariki wakati wa tendo la ndoa na mwanamke ambae polisi wamethibitisha kuwa ana umri wa miaka 25, kwa mujibu wa polisi mwanaume huyo alikua na umri wa miaka 55.
Inasemekana kuwa mwanaume huyo ndiye alikua wa kwanza kuwasili na kulipia chumba chao cha hoteli huku mwanamke huyo akijiunga nae badae, katika tarifa aliyoandikisha na polisi mwanamke huyo alisema mwanaume huyo alipozimia hakua na budi kuarifu wasimamizi wa hoteli na ndipo hapo polisi waliarifiwa kuhusu tukio hilo na hatimae mwanamke huyo kutiwa mbaroni.