Akiri kuwauwa watu 14, amuomba Hakimu amlinde

Mshukiwa wa mauaji Denis Kazungu (34), amekiri mbele ya Mahakama ya Kicukiro mjini Kigali nchini Rwanda kwamba aliwaua watu 14, wengi wao wakiwa wanawake na mwanamume mmoja.

Kazungu pia amesema, licha ya kutokuwa na ushahidi wowote, aliwaua watu hao kwa sababu anahisi walimwambukiza kwa makusudi Virusi vya UKIMWI na kwamba pamoja na mauaji, pia alibaka na kuiba. 

Hata hivyo, majina ya wahanga wa muuaji huyo hayajafahamika na ameiomba kesi hiyo isiwekwe hadharani, ili kuepusha kuzua hasira na hamasa kwa watu wengine kumfuata na kumdhuru.

Awali, mbele ya Mahakama upande wa upelelezi ulidai mshukiwa huyo alikuwa akiwarubuni watu katika migahawa na kuwapeleka hadi nyumbani kwake katika kitongoji cha Busanza mjini Kigali, na kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Jumanne ijayo Septemba 24, 2023.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii