Chelsea wamemsajili Romeo Lavia kutoka Southampton

Chelsea imetangaza kumsajili kiungo, Romeo Lavia kutoka Southampton kwa mkataba wa awali wenye thamani ya pauni milioni 53 pamoja na nyongeza za pauni milioni 5.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amesaini mkataba wa miaka saba hadi 2030 na klabu hiyo ya West London.

"Siwezi kusubiri kukutana na wachezaji wenzangu wote wapya na kujenga kemia pamoja ili kufikia mambo mazuri pamoja."

Lavia alijiunga na Southampton kutoka Manchester City mwaka wa 2022. Alicheza mechi 34 kwa Saints katika msimu wake wa kwanza.

Chelsea wametumia Euro milioni 386 kwa uhamisho wa majira ya joto hadi sasa, ikiwa ni pamoja na ada ya rekodi ya Uingereza ya £115m kwa Moises Caicedo kutoka Brighton.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii