Beki kutoka nchini England Harry Maguire ameuvimbia Uongozi wa Manchester United akitaka alipwe Pauni 15 Milioni kwanza, kabla ya kukubali kwenda kujiunga na West Ham United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Mabosi wa klabu hiyo ya Old Trafford walidhani kwamba wameshamaliza kila kitu kuhusu beki huyo wa kati baada ya kukubali ofa ya Pauni 30 milioni kutoka kwa Wagonga Nyundo hao wa London.
Uongozi wa Man Utd ulikuwa tayari kumlipa Maguire Pauni 6 Milioni ili aondoke klabuni hapo, lakini imekuwa tofauti na ilivyofikiriwa.