Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Yacouba Songne ameaga rasmi Ihefu SC, baada ya kukamilisha mpango wa kusajiliwa na Arta Solar 7 ya Djibout.
Yacouba alijiunga Ihefu FC wakati wa Dirisha Dogo la Usajili msimu uliopita akitokea Young Africans, na aliiisaidia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo ya mkoani Mbeya katika Kampeni zake za kutokushuka daraja.
Kiungo huyo aliyewahi kuitumikia Asante Kotoko ya Ghana ameaga Ihefu FC kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, akiandika maneno mazito na yenye faraja kwa Mashabiki, Uongozi na Wachezaji wenzake ambao amewaacha klabuni hapo.